POLICE FC YALENGA UBINGWA MSIMU MPYA
Kenya Police FC imefanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake ikiwa na lengo la kuwania ubingwa wa Ligi ya SportPesa na Kombe la Mozzart Bet baada ya kumaliza msimu uliopita bila taji.
Klabu hiyo imefanya mabadiliko 29 katika dirisha la usajili, ikisajili wachezaji 11 na kuwaachilia 18, huku kocha Nicholas Muyoti akisema amefika katika klabu hiyo akiwa na jukumu la kutafuta matokeo badala ya kupewa muda wa kusubiri.
Police FC imelenga kuimarisha ushindani ndani ya kikosi na kupunguza pengo dhidi ya mabingwa Gor Mahia, huku wachezaji wapya wakitarajiwa kuongeza nguvu katika maeneo mbalimbali ya timu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































