#Local News

KENYA IMEELEZEA DHAMIRA YAKE YA KUZINGATIA USALAMA WA NYUKLIA

Kenya imeeleza dhamira yake ya kuzingatia usalama wa nyuklia, huku serikali ikijiandaa kujenga kiwanda cha kwanza cha nguvu za nyuklia katika Kaunti ya Siaya.

Waziri wa Afya Aden Duale amesema Kenya imepiga hatua katika maandalizi ya mradi huo wa thamani ya shilingi bilioni mia tano. Alizungumza hayo katika mkutano wa IAEA mjini Vienna, Austria.

Duale amesema ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kuanza mwaka 2027, huku kikitarajiwa kuunganishwa na gridi ya taifa ifikapo mwaka 2034.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *