CHARLES OWINO AITAKA IEBC KUCHUKUA HATUA DHIDI YA HASSAN OMAR
Msemaji wa Serikali Charles Owino ameitaka IEBC kuchukua hatua kali dhidi ya Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar kufuatia kauli zake kuhusu matumizi ya wapiga kura waliofariki katika uchaguzi wa 2027.
Owino amesema kauli hiyo ni ya uzembe na haikutarajiwa kutoka kwa kiongozi wa chama tawala, akisema inaweza kuongeza hofu na kufanya mazingira ya kisiasa kuwa tete kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao.
Amesema Hassan Omar anapaswa kuwajibika binafsi kwa kauli zake, huku akisisitiza kuwa IEBC ina jukumu la kuchukua hatua kali dhidi ya matamshi yanayoweza kutikisa imani ya wananchi katika mchakato wa uchaguzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































