RUTO APENDEKEZA KISUMU AIRPORT IITWE RAILA ODINGA INTERNATIONAL AIRPORT
Rais William Ruto amependekeza kubadilishwa kwa jina la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu na kuitwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Raila Odinga, kama sehemu ya mipango ya kumuenzi aliyekuwa Waziri Mkuu.
Ruto amesema mashauriano yanaendelea na serikali ya Kaunti ya Kisumu pamoja na wakazi wa eneo hilo kuhusu pendekezo hilo, akisema uamuzi huo ni sehemu ya juhudi za kuheshimu mchango wa Raila Odinga.
Rais pia amethibitisha kuwa Uwanja wa Talanta jijini Nairobi utaitwa Uwanja wa Kimataifa wa Raila Odinga utakapofunguliwa rasmi, hatua nyingine ya kumuenzi mwanasiasa huyo aliyefariki mwaka 2025.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































