JOHN KORIR ALENGA REKODI YA CHINI YA SAA MBILI VALENCIA MARATHON
Bingwa mara mbili wa Boston Marathon John Korir ameweka lengo la kuandika historia Desemba 6 kwa kulenga kuvunja muda wa saa mbili katika mbio za Valencia Marathon nchini Uhispania.
Korir anaamini njia ya Valencia ni miongoni mwa zenye kasi zaidi duniani na inampa nafasi nzuri ya kujaribu kufikia rekodi hiyo, baada ya Sebastian Sawe kuwa mwanariadha wa kwanza rasmi kukimbia kilomita 42 chini ya saa mbili kwa muda wa 1:59:30 London Marathon.
Korir amesema atafurahia muda wowote atakaopata Valencia, lakini dua yake kubwa ni kukimbia chini ya saa mbili, akiamini bado ana uwezo wa kufuata nyayo za Sawe na kuingia katika vitabu vya historia ya riadha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































