#Local News

IEBC YAMWITA HASSAN OMAR KUFUATIA KAULI ZA WAPIGA KURA WALIOFARIKI

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imemwita Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar kufuatia kauli zake kuhusu madai ya matumizi ya wapiga kura waliofariki katika uchaguzi wa 2027.

Kamishna wa IEBC Alutalala Mukhwana amesema kauli hizo zinaweza kuzua hofu na mashaka miongoni mwa wananchi kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao, akisisitiza umuhimu wa kulinda imani ya umma katika mchakato wa uchaguzi.

Kauli ya IEBC imejiri wakati Waziri Mkuu wa Kwanza Musalia Mudavadi akisema Rais William Ruto hatatumia njia za mkato kushinda uchaguzi, huku akisisitiza kuwa ushindi utapatikana kupitia mchakato halali wa kidemokrasia.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *