#Local News

RUTO KUENDELEZA ZIARA YA MAENDELEO SIAYA LEO

Rais William Ruto anatarajiwa kuendeleza ziara yake ya maendeleo katika Kaunti ya Siaya hii leo akiwa na ratiba ya kukagua barabara na madaraja, pamoja na miradi ya nyumba za bei nafuu

Ziara hiyo ni seAhemu ya safari yake ya siku nne katika Nyanza, baada ya kukamilisha siku mbili za shughuli mbalimbali Kisumu ambako alizindua miradi mikubwa ya miundombinu na kufanya mikutano ya kisiasa

Ruto pia anatarajiwa kukutana na wakazi pamoja na viongozi wa Siaya, huku ziara hiyo ikija wakati serikali ikizidisha shughuli za maendeleo na kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *