#Local News

GAVANA WA MOMBASA AMEAGIZA KUAJIRIWA KWA WAHUDUMU WAPYA WA AFYA

Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Nassir, ameagiza kuajiriwa kwa wahudumu wapya wa afya ili kuongeza idadi ya wafanyakazi katika vituo vya matibabu vya kaunti hiyo.

Gavana Nassir amesema hatua hiyo inalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya na kupunguza changamoto ya upungufu wa wahudumu katika hospitali na vituo vya afya.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati sekta ya afya ikikabiliwa na changamoto mbalimbali, huku serikali za kaunti zikiendelea kutafuta njia za kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *