#Local News

NPS IMEWAPONGEZA WAKENYA KWA KUDUMISHA AMANI WAKATI WA MKUTANO WA LINDA MWANANCHI NAIROBI

Huduma ya Kitaifa ya Polisi, NPS, imewapongeza Wakenya kwa kudumisha amani wakati wa mkutano wa kisiasa wa Linda Mwananchi, uliofanyika Jumapili katika uwanja wa Jacaranda, Embakasi, Nairobi.

NPS imesema waandalizi, washiriki na maafisa wa usalama walishirikiana kwa kuheshimiana na kujizuia na vitendo vya vurugu.

Polisi imesema mkutano huo unaonyesha umuhimu wa Wakenya kutumia haki zao za kikatiba kwa amani na kwa kufuata sheria.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *