#Local News

RUTO AMKOSOA UHURU BAADA YA UAMUZI WA MAHAKAMA

Rais William Ruto amemsuta tena aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, akimkosoa kwa kuendelea kujihusisha na siasa za upinzani badala ya kuchukua nafasi ya kuwa kiongozi mstaafu anayesimamia umoja wa taifa.

Akizungumza Kaunti ya Siaya Ruto ameunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu unaowazuia marais wastaafu kushikilia nyadhifa za uongozi katika vyama vya kisiasa zaidi ya miezi sita baada ya kuondoka madarakani.

Ruto pia amewataka Wakenya kuwa na tahadhari dhidi ya viongozi wa upinzani, akidai wanacheza kamari na mustakabali wa Kenya, huku akiendelea kuhamasisha uungwaji mkono wa serikali yake kuelekea uchaguzi wa 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *