#Football #Sports

LIVERPOOL YAWATOA TOTTENHAM KOMBE LA LIGI KWA KICHAPO CHA 3-1

Liverpool imeichapa Tottenham 3-1 katika raundi ya tatu ya Kombe la Ligi, huku Alexis Mac Allister, Cody Gakpo na Dominik Szoboszlai wakifunga mabao kwa Liverpool katika ushindi uliotokea Uwanja wa Anfield.

Tottenham iliyokuwa imeanza vibaya msimu wa Ligi Kuu ilishindwa kutumia mashindano hayo kujipa matumaini mapya, huku Liverpool ikitawala mchezo licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha jijini Liverpool.

Kwa Upande wao Arsenal iliichapa Ipswich 4-2 katika raundi ya tatu ya Kombe la Ligi, huku kinda wa miaka 16 Max Dowman akivutia katika mechi yake ya kwanza msimu huu.

Dowman alimwonyesha kocha Mikel Arteta uwezo wake mapema dakika ya saba, akitumia kasi yake kuwapita walinzi kabla ya kufunga kwa utulivu bao la tatu la Arsenal.

Bao hilo lilikuwa la pili kwa Dowman akiwa Arsenal baada ya kufunga dhidi ya Everton mwezi Machi, huku kiwango chake kikiendelea kuibua matarajio makubwa kuhusu mustakabali wake katika kikosi hicho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *