WAKENYA WAWIKA BERLIN
Wakenya walitangaza umahiri wao jijini Berlin kwenye mbio za Half Marathon, kutokana na kasi yao ya kuridhisha kwenye mbio hapo jana.
Andrea Kiptoo alimaliza wa kwanza katika mbio za wanaume kwa muda wa dakika 59:11, sekunde 3 pekee mbele ya mkenya mwenzake Dennis Kipkemoi, huku Mjerumani Amanal Petros akifunga nafasi tatu bora.
Katika mbio za wanawake, Likina Amebaw wa Ethiopia alimaliza wa kwanza katika muda wa 1:05.07, Ethiopia ikitawala nafasi 3 za kwanza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































