INGWE WAKWARUZA ULINZI, WAWEKA HAI MATUMAINI YA UBINGWA
Matumaini ya Ulinzi Stars kujiondoa katika eneo la kushushwa daraja yalizimwa jana baada ya kukwaruzwa na AFC Leopards kwa kichapo cha mabao 2-0 na kuwaacha wanajeshi hao miongoni mwa timu 3 ambazo sasa zinakabiliwa na hatari ya kuiaga ligi kuu ya soka, KPL mwishoni mwa msimu.
Shambulizi la kiungo wa Rising Stars Kelly Madada katika dakika ya 43 na bao la Emmanuel Lwangu kunako dakika ya 82 yaliweka hai matumaini ya Ingwe kunyakua ubingwa wa ligi hiyo ambao umewakwepa tangu mwaka wa 1998.
Zikiwa zimesalia mechi 3 kabla ya ligi kutamatika, Ingwe wanawaandama viongozi Gor Mahia wakiwa na pointi 61, nao Gor wakiwa na pointi 65.
Maombi ya Gor na Leopards yatakuwa njia ya mshindani iwe giza na utelezi, Gor wanaposaka ubingwa wa kihistoria wa ligi hiyo kwa mara ya 22.
Leopards walionyesha mchezo wa kuridhisha katika vipindi vyote viwili vya mchezo huo, ambao utawapa wafuasi matumaini na ari ya kutwaa taji hilo la KPL na kukata kiu ya zaidi ya miaka 28.
Kwenye matokeo mengine, matumaini ya Shabana FC kumaliza katika nafasi ya 3 bora yalididimia hapo jana, kufuatia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mara Sugar.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































