VIONGOZI WA ODM WAAPA KUSIMAMA NA RUTO HADI 2027
Viongozi wa ODM katika eneo la Nyanza wameendelea kuunga mkono ushirikiano wao na Rais William Ruto, wakisema maendeleo yanayoendelea kutekelezwa katika eneo hilo ndiyo msingi wa msimamo wao wa kufanya kazi na serikali.
Wakiongozwa na Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga viongozi hao wametoa hakikisho la kushirikiana na Rais Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, wakisema kuwa hakutakua na mazungumzo na mrengo mwingine wa kisiasa.
Viongozi hao wameeleza kuwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa Nyanza imeimarisha uhusiano wao na serikali, huku Ruto akisema uwekezaji wa serikali katika eneo hilo unalenga kuhakikisha maendeleo yanafika katika maeneo yote ya nchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































