AMISI ADAI KUTIMULIWA LINDA MWANANCHI KWA MGOGORO WA CHAMA
Mbunge wa Saboti Caleb Amisi anadai aliondolewa katika makundi ya WhatsApp ya vuguvugu la Linda Mwananchi kufuatia kutokubaliana kuhusu chama kitakachotumika kama chombo cha kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027
Amisi alikuwa akijibu kauli za Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kuhusu vyama mbalimbali vilivyojadiliwa na viongozi wa Linda Mwananchi, akimshukuru Owino kwa kuthibitisha kuwa chama chake cha Political Movement ndicho kilichoanzishwa awali kulibeba vuguvugu hilo
Amisi aidha anadai baadhi ya watu walijiunga baadaye na kuingilia nafasi ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, huku yeye mwenyewe akiondolewa katika makundi ya WhatsApp ya Linda Mwananchi
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































