UHURU AKUBALI KUACHA UONGOZI WA JUBILEE BAADA YA UAMUZI WA MAHAKAMA
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa ataachia nafasi ya kiongozi wa Chama cha Jubilee kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu unaowazuia marais wastaafu kushikilia nyadhifa za uongozi katika vyama vya kisiasa zaidi ya miezi sita baada ya kuondoka madarakani
Kupitia Katibu wake wa Mawasiliano Kanze Dena, Uhuru amesema alibaki katika uongozi wa Jubilee kutokana na mzozo wa muda mrefu wa ndani ya chama uliokuwa ukihitaji ufafanuzi wa kisheria.
Uhuru amesema anaheshimu uamuzi huo na kuutaja kama hatua inayoimarisha utawala wa sheria na demokrasia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































