CARRICK ATAKA UNITED ITUMIE HASIRA YA DABI KUMKABILI BRIGHTON
Kocha wa Manchester United Michael Carrick amewataka wachezaji wake kutumia hasira na maumivu ya kupoteza dhidi ya Manchester City kama motisha ya kurejea katika njia ya ushindi dhidi ya Brighton kwenye Kombe la Ligi.
United ilishindwa kutumia faida ya City kubaki na wachezaji 10 baada ya Phil Foden kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza, kabla Erling Haaland kufunga bao la ushindi dakika ya 60 katika mchezo uliogubikwa na utata wa maamuzi ya waamuzi.
Carrick amesema kikosi chake lazima kisahau kichapo hicho na kuelekeza nguvu kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la Ligi dhidi ya Brighton usiku wa leo, kikilenga kurejesha matumaini baada ya matokeo ya dabi ya Manchester.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































