#Local News

MUDAVADI AMETOA WITO WA ULINZI WA WAKENYA WANAOFANYA KAZI NJE YA NCHI

Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ametoa wito wa kuimarishwa kwa ulinzi wa Wakenya wanaofanya kazi nje ya nchi, kupitia mifumo bora ya kuwasajili na mikataba thabiti kati ya nchi.

Mudavadi pia ametaka kuwepo kwa ushirikiano wa kisheria kati ya nchi na njia rahisi za kutatua migogoro ya wafanyakazi.

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Strathmore jijini Nairobi, Mudavadi amesema Wakenya wanaofanya kazi nje ya nchi wanapaswa kupata haki bila kujali nchi wanakofanyia kazi.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *