CARRICK AJIPA LAWAMA BAADA YA UNITED KUPOROMOKA OLD TRAFFORD
Kocha wa Manchester United Michael Carrick amejilaumu baada ya timu yake kupoteza 3-2 dhidi ya Brighton katika Kombe la Ligi, licha ya kuongoza kwa mabao mawili mapema katika mchezo huo wa raundi ya tatu.
Shea Lacey na Mason Mount waliiweka United mbele kwa mabao mawili ndani ya dakika kumi za kwanza, kabla Charalampos Kostoulas, Pascal Gross na Maxim De Cuyper kugeuza mechi na kuipa Brighton ushindi.
Mashabiki wa United waliwazomea wachezaji na benchi la ufundi baada ya kipenga cha mwisho, huku Carrick akisema kushindwa katika mechi sio jambo linalokubalika na kuchukua sehemu kubwa ya lawama.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































