#Local News

GAVANA BARASA AMEKASHIFU UPINZANI KUHUSU KUTAKA KITUO CHA KUJUMUISHA KURA KIONDOLEWE

Gavana wa Kakamega, Fernandes Barasa, amekashifu wito wa baadhi ya viongozi wa upinzani wanaotaka kituo kikuu cha kujumuishia kura za urais kiondolewe. Barasa amesema hatua hiyo inaweza kuathiri mchakato wa uchaguzi.

Gavana huyo amewataka viongozi wa kisiasa kuunga mkono taratibu zilizowekwa na taasisi zinazosimamia uchaguzi. Amesema ni muhimu wananchi kuwa na imani na mchakato wa uchaguzi.

Kauli ya Barasa inajiri wakati taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu ujao, huku mjadala kuhusu namna kura za urais zitakavyohakikiwa na kutangazwa ukiendelea.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *