#Sports

RUTO APEWA SIFA KWA KUISAIDIA KENYA KUPATA MWENYEJI WA WORLD ATHLETICS 2029

Mwenyekiti wa Kamati ya Zabuni ya Nairobi 2029 Ibrahim Hussein amesema Rais William Ruto alitoa mchango muhimu katika kampeni iliyoiwezesha Kenya kushinda zabuni ya kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha ya 2029, yaliyotwaliwa na Nairobi baada ya kushindana na miji kadhaa ya Ulaya.

Hussein amesema ujumbe wa video uliorekodiwa na Ruto kwa Baraza la Riadha Duniani, akiahidi serikali kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa, ulitolewa wakati muhimu na kuipa Kenya msukumo katika mchakato wa zabuni.

Uamuzi huo uliotangazwa na Rais wa Riadha Duniani Sebastian Coe unafanya Nairobi kuwa mwenyeji wa kwanza barani Afrika kuandaa Mashindano ya Dunia ya Riadha, hatua iliyofikiwa baada ya kampeni iliyolenga kuonyesha uwezo wa Kenya kuandaa mashindano ya kiwango cha kimataifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *