#Local News

VIJANA ZAIDI YA 120,000 WAFUNGWA KWA MAKOSA YA VURUGU NCHINI

Zaidi ya vijana 120,000 wamefungwa nchini Kenya kati ya mwaka 2022 na 2026 kwa makosa yanayohusiana na vurugu, kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen.

Kati ya idadi hiyo, vijana 11,824 wamehukumiwa kifungo kwa makosa yakiwemo uhalifu wa magenge, itikadi kali za kigaidi na vitendo vya kihuni, huku serikali ikisema visa hivyo vinaendelea kuwa changamoto kwa usalama.

Murkomen amesema serikali inaongeza juhudi za kudumisha usalama kote nchini, huku ikiendelea kuchukua hatua dhidi ya makundi na watu wanaohusika katika vitendo vya vurugu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *