#Local News

WAFANYAKAZI WA ANGA WAPINGA VITISHO VYA MIGOMO YA KAWU

Mgawanyiko umeibuka miongoni mwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga nchini, huku baadhi yao wakipinga vitisho vya mara kwa mara vya mgomo vinavyotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Anga Kenya, KAWU.

Wafanyakazi hao, wengi wao kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya, wamesuta uongozi wa chama hicho kwa kuchochea mvutano wa kikazi na kuitaka KAWU kutanguliza mazungumzo katika kutatua mizozo badala ya vitisho vya migomo vinavyoweza kuvuruga shughuli za viwanja vya ndege.

Wameitaka KAWU kuzingatia maslahi ya wafanyakazi, usalama wa ajira na mazingira ya kazi, huku wakitaka pia uongozi wa mamlaka hiyo kushughulikia malalamishi yaliyosalia.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *