KINDIKI NA MUDAVADI WATOA UHAKIKISHO KUHUSU UCHAGUZI WA 2027
Serikali imewahakikishia Wakenya na washirika wa maendeleo kuwa uchaguzi mkuu wa 2027 utafanyika kwa wakati kwa mujibu wa Katiba, wakati baadhi ya viongozi wa upinzani wakiendelea kuibua wasiwasi kuhusu maandalizi ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka
Naibu Rais Kithure Kindiki amesema hakutakuwa na njia za mkato katika mchakato wa uchaguzi, akiwataka washirika wa maendeleo wanaotaka kusaidia demokrasia kufanya hivyo kupitia taasisi na njia zilizowekwa kisheria
Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi ameunga mkono msimamo huo akisema Kenya ina utamaduni wa kufanya uchaguzi kwa mujibu wa ratiba ya Katiba.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































