#Football #Sports

GOR MAHIA YAANZA UTETEZI WA UBINGWA DHIDI YA MURANG’A SEAL

Mabingwa wa Ligi ya SportPesa Gor Mahia wataanza rasmi kampeni ya kutetea taji hilo dhidi ya Murang’a Seal katika Uwanja wa Nyayo Jumamosi saa kumi jioni, huku kocha Charles Akonnor akitaka kikosi chake kuwa makini baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gor Mahia iliondolewa na Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 7-1, baada ya kupoteza 2-0 jijini Nairobi kabla ya kuchapwa 5-1 nchini Misri, matokeo yaliyomkera Akonnor kutokana na makosa ya msingi ya kiulinzi.

Akonnor sasa amewataka wachezaji wake kuamka na kurekebisha makosa hayo wanapoelekeza nguvu katika ligi, huku Gor Mahia ikilenga kuanza vyema harakati za kutetea ubingwa wake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *