#Local News

RUTO AMLENGA UHURU, ASEMA UCHAGUZI WA 2027 UTALENGA UMOJA

Rais William Ruto ameongeza ukosoaji wake dhidi ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akidai kuwa anafadhili viongozi wa upinzani kwa lengo la kudhoofisha serikali yake.

Akizungumza Migori katika siku ya nne ya ziara yake ya Nyanza, Ruto amesema uchaguzi mkuu wa 2027 utazingatia umoja wa kitaifa na ushirikishwaji, akitofautisha mtazamo huo na kile alichokitaja kuwa siasa za mgawanyiko za tawala zilizopita.

Ruto pia ametumia ziara hiyo kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya mabilioni ya shilingi katika Kaunti ya Migori, huku akisisitiza utekelezaji wa miradi hiyo kwa wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *