MGOGORO WA UONGOZI WAZIDI KUIYUMBUA LINDA MWANANCHI
Mvutano wa kisiasa unazidi kuigawanya kambi ya Linda Mwananchi huku baadhi ya wanachama wakiegemea vyama tofauti wanapojiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2027.
Mbunge wa Embakasi Mashariki na anayewania ugavana wa Nairobi Babu Owino amesema kuna mvutano unaozidi kushika kasi ndani ya kambi hiyo.
Owino amesema anaunga mkono Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwania urais, lakini ameeleza kuwa atahudhuria baadhi tu ya mikutano ya Linda Mwananchi huku akisisitiza kuwa kambi hiyo inahitaji kuelewana kuhusu mwelekeo wake wa kisiasa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































