#Local News

VIONGOZI WA ODM MOMBASA WAMEMKOSOA HASSAN OMAR KWA MATAMSHI YA KUWAGAWANYA WANACHI

Viongozi wa ODM Mombasa wamemkosoa Hassan Omar kwa matamshi ambayo wameyataja kuwa ya kugawanya wananchi. Viongozi hao wamesema kauli hizo zinaweza kuleta tofauti na mvutano miongoni mwa wakazi wa Mombasa.

Wamewataka viongozi wa kisiasa kutumia lugha ya amani na kuzingatia umoja wa wananchi. Wamesema siasa inapaswa kujengwa kwa hoja na maendeleo, badala ya kauli zinazoweza kuwagawa watu.

Hassan Omar bado hajajibu kwa kina kuhusu ukosoaji huo. Sakata hilo linaendelea kufuatiliwa huku viongozi na wananchi wakihimizwa kudumisha amani na mshikamano.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *