CHELSEA, ARSENAL NA UNITED KATIKA MIKIKIMIKIKI YA LIGI KUU ENGLAND
Ligi Kuu ya Uingereza inaendelea leo usiku huku Brentford ikiikaribisha Chelsea saa nne usiku, kabla ya michezo mitano kuchezwa Jumamosi ikiwemo Tottenham dhidi ya Aston Villa na Brighton dhidi ya Arsenal.
Jumamosi pia Everton itacheza na Ipswich Town, Newcastle ikikabiliana na Hull City huku Nottingham Forest ikiikaribisha Coventry, kabla ya Jumapili Bournemouth kucheza na Liverpool, Manchester City dhidi ya Sunderland na Leeds kukutana na Crystal Palace.
Ratiba hiyo itafungwa Jumapili saa kumi na mbili unusu wakati Fulham ikikaribisha Manchester United, huku michezo hiyo ikitarajiwa kuongeza ushindani katika mbio za msimu huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































