KUPPET YATAKA KUSITISHWA KWA MAJADILIANO YA MISWADA YA ELIMU
Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kati KUPPET kimeitaka serikali kusitisha kwa muda mikutano ya umma kuhusu miswada sita ya elimu, ikiwemo Mswada wa Elimu ya Msingi wa 2026 na Mswada wa Elimu ya Juu na Ufadhili.
KUPPET imesema mchakato huo unafanywa kwa haraka na haujahusisha wadau wote kwa kiwango cha kutosha, hivyo kutaka muda zaidi utolewe ili wananchi na wahusika wengine washiriki kikamilifu.
Wakati huo huo, Seneta wa Kiambu Karungo Wa Thang’wa ameibua wasiwasi kuhusu mfumo unaopendekezwa wa ufadhili wa elimu ya juu, akisema mswada huo haujaweka wazi chanzo cha fedha za Mamlaka ya Ufadhili wa Elimu ya Juu wala masharti ambayo wanafunzi watatumia kukopa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































