#Sports

VIKAPU: KPA YASHIKA USUKANI BAADA YA KUICHAPA EQUITY 102-87

KPA imepiga hatua kuelekea fainali ya Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu nchini baada ya kuichapa Equity Bank 102-87 katika mchezo wa pili wa nusu fainali uliofanyika Nyayo Gymnasium.

KPA ilianza kwa kusuasua na kuruhusu Equity kuongoza kwa tofauti ya pointi 10, kabla ya kurejea mchezoni na kuimarika hadi kufunga mchezo kwa kasi kubwa katika robo ya nne.

Ushindi huo umeipa KPA uongozi wa 2-0 katika mfululizo wa michezo mitano, hivyo inahitaji ushindi mmoja pekee kufuzu fainali, huku Equity ikilazimika kushinda mchezo unaofuata ili kuendelea kuwa na matumaini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *