MASAIBU YA UNITED YAZIDI KIWANGO
Masaibu yameendelea kurundika uga wa Old Trafford baada ya Manchester United kupewa kichapo cha mabao 2-1 na Brighton na hivyo kubanduliwa nje ya kombe la FA katika raundi ya 3 hapo jana, ikiwa ni mara ya kwanza kwa United tangu msimu wa 1981-82 kubanduliwa nje ya Carabao Cup na FA Cup katika awamu za mwanzo.
Mabao ya Brajan Gruda na mshambulizi wao wa zamani Danny Welbeck yalihakikisha United wanacheza mechi 40 pekee msimu huu, zikiwa 2 za FA na Carabao, na 38 za ligi kuu.
Benjamin Sesko alifunga bao dakika ya 85, ila hilo halikuwazuia United kubanduliwa, ingawa kichapo hicho kitawapa fursa ya kusaka nafasi ya kurejea katika mashindano ya bara Ulaya msimu ujao.
Huenda ikawa mechi ya mwisho kwa Darren Fletcher, kocha wa zamani wa United Ole Gunnar Solskjaer na Michael Carrick wakipigiwa upato kuchukua mikoba kutoka Ruben Amorim aliyetimuliwa.
Droo ya raundi ya 4 itafanyika leo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































