KOCHA WA TUSKER AKIRI UBINGWA UMEWAPONYOKA
Kocha mpya wa Tusker FC, Julien Mette, amekiri kuwa timu hiyo haina tena nafasi ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya SportPesa msimu huu.
Mette amesema sasa wataelekeza juhudi katika kuhakikisha wanamaliza katika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi, pamoja na kuwania kombe la mashindano ya ndani.
Licha ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Shabana FC katika Uwanja wa Gusii, kocha huyo amewasifu wachezaji wake kwa kiwango kizuri walichoonyesha. Bao la Thomas Teka liliipa Shabana alama zote tatu katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































