#Athletics #Sports

GABBY THOMAS AWASILI KENYA KABLA YA KIP KEINO CLASSIC

Nyota wa riadha kutoka Marekani Gabby Thomas amewasili nchini Kenya tayari kwa mashindano ya Kip Keino Classic ambapo sasa atashiriki mbio za mita mia moja na mita mia mbili

Mkurugenzi wa mashindano hayo Barnaba Korir amethibitisha kuwa Thomas tayari ameanza mazoezi yake nchini kabla ya mashindano yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa Aprili ishirini na nne katika Uwanja wa Nyayo

Uamuzi wake wa kushiriki mbio mbili badala ya moja umeongeza msisimko mkubwa katika mashindano hayo huku waandaaji wakitarajia ushindani mkali na mvuto wa kimataifa katika mbio za wanawake ambazo zimevutia wanariadha bora kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *