#Athletics #Sports

RUTO AIPONGEZA TIMU KENYA KWA MAFANIKIO GLASGOW

Rais William Ruto ameipongeza Timu Kenya kwa kufanya vyema katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 2026 iliyofanyika Glasgow, Scotland, baada ya kumaliza miongoni mwa mataifa yaliyofanya vizuri zaidi.

Kenya ilishika nafasi ya 12 kwa jumla baada ya kujizolea medali 12, zikiwemo tatu za dhahabu, nne za fedha na tano za shaba, hatua inayodhihirisha uwezo wa wanamichezo wa nchi katika mashindano ya kimataifa.

Katika ujumbe wake, Rais Ruto amewapongeza wanariadha kwa kujituma na kuipeperusha vyema bendera ya Kenya, akisema mafanikio yao yameliletea taifa heshima na fahari kubwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *