CHELSEA WAMZAWADIA JOÃO PEDRO MKATABA MPYA
Chelsea wanatarajiwa kumzawadia João Pedro mkataba mpya wa muda mrefu baada ya kufikia makubaliano ya awali kuhusu kuongeza muda wake wa kusalia klabuni hadi Juni 2033.
Ripoti zinaeleza kuwa mkataba huo pia utajumuisha nyongeza ya mshahara, baada ya Chelsea kukataa majaribio ya klabu tatu kubwa zilizokuwa zikimtaka mchezaji huyo.
Hatua hiyo inaonyesha imani kubwa ya Chelsea kwa João Pedro, ambaye anaendelea kuhesabiwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































