#Local News

SERIKALI YATIA SAINI MKATABA WA KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO

Mapambano dhidi ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga yamepata msukumo mpya baada ya serikali kupata ufadhili wa kuimarisha huduma za afya nchini.

Wizara ya Afya imetia saini mkataba wa ushirikiano na Beginnings Fund utakaowezesha kupatikana kwa shilingi bilioni 10.3 za kufadhili mpango wa miaka mitano wa kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Waziri wa Afya Aden Duale amesema ushirikiano huo utaimarisha miundombinu ya afya ya uzazi na kusaidia kufanikisha lengo la kupunguza hadi kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *