#Football #Sports

HARAMBEE STARLETS YAAGA KOMBE LA WAFCON

Safari ya Kenya katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake imefikia tamati baada ya kikosi hicho kushindwa kuvuka hatua ya makundi.

Harambee Starlets imeaga Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) baada ya kufungwa mabao 2-0 na Algeria katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A uliochezwa jijini Rabat, Morocco.

Starlets imemaliza mashindano bila pointi, huku mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Marine Dafeur na Lynda Bendris yakiihakikishia Algeria tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *