ODM YAMUUNGA MKONO RUTO KWA MUHULA WA PILI
Mwelekeo wa siasa za mwaka 2027 umechukua sura mpya baada ya uamuzi wa ODM kuhusu uchaguzi ujao, hatua inayotarajiwa kuzua mjadala ndani na nje ya chama hicho.
Kiongozi wa ODM Oburu Oginga ametangaza kuwa chama hicho kitamuunga mkono Rais William Ruto kuwania muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 badala ya kusimamisha mgombea wake wa urais.
Oburu pia ametangaza nia ya kuwania nafasi ya Naibu Rais, akisema wadhifa huo bado uko wazi kwa mazungumzo, hatua inayofungua ushindani ndani ya ODM baada ya Junet Mohamed kumpendekeza Wycliffe Oparanya kwa nafasi hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































