#Local News

RUTO AKOSOA UPINZANI KWA KUPINGA MAZUNGUMZO YA DIRA YA 2060

Mjadala kuhusu mazungumzo ya kitaifa ya Dira ya 2060 unaendelea kushika kasi huku Rais William Ruto akiitaka upinzani kushiriki katika mchakato huo badala ya kuupinga.

Ruto ameukosoa upinzani kwa kupinga mazungumzo ya kitaifa kuhusu Dira ya 2060, akisema mchakato huo unalenga kuweka mkakati wa kuifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa yaliyoendelea kiuchumi.

Aidha  amemtaka mgombea wa urais wa upinzani kujitokeza na kumkabili katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, akisema Wakenya watachagua rais wao kwa kuzingatia uwezo wa uongozi na si kauli za kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *