#Football #Sports

ST. JOSEPH’S GIRLS KITALE YATWAA TAJI LA TAIFA KWA SOKA LA WASICHANA

St. Joseph’s Girls Kitale imetwaa ubingwa wa taifa wa soka ya wasichana wa shule za upili baada ya kuibuka na ushindi katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa M-Pesa Foundation Academy mjini Thika.

St. Joseph’s Girls, chini ya kocha Francis Ojillo, ilitwaa taji lake la kwanza la kitaifa kwa kuishinda Nyakach Girls kwa mikwaju ya penalti 7-6, baada ya sare ya 1-1 iliyodumu hadi mwisho wa muda wa nyongeza.

Nyakach Girls ilitangulia kufunga kupitia Iddah Matara, kabla ya Mirriam Silali kusawazisha kwa St. Joseph’s Girls na kuupeleka mchezo huo katika muda wa nyongeza na hatimaye mikwaju ya penalti, ambapo timu ya JOGA  iliibuka mabingwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *