WANAWAKE ISIOLO WAACHA UCHOMAJI MAKAA
Wanawake katika Kaunti ya Isiolo wameacha biashara ya uchomaji mkaa na kuhamia ufugaji na biashara ya mbuzi kama njia ya kulinda mazingira na kujipatia kipato.
Wanawake hao wanasema uchomaji mkaa ulikuwa chanzo kikuu cha mapato lakini ulichangia uharibifu wa misitu na kuongezeka kwa changamoto za kimazingira. Kupitia biashara ya mbuzi, sasa wamepata njia mbadala ya kujikimu huku wakihifadhi mazingira.
Wameitaka serikali na mashirika ya maendeleo kuendelea kuwaunga mkono kwa mafunzo na rasilimali ili kuimarisha biashara hiyo na kuwahamasisha wanawake zaidi kuachana na shughuli zinazoharibu mazingira.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































