RIGATHI ASHTUMU DCI KWA KUFICHA USHAHIDI DHIDI YA KIFO CHA VICTORIA MUTISO
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amemshutumu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Mohamed Amin kwa kuficha madai ya kuhusika kwa polisi katika mauaji ya Victoria Mutiso.
Gachagua amedai kuwa kuna maswali ambayo hayajajibiwa kuhusu nafasi ya maafisa wa polisi katika kifo cha Mutiso akisisitiza kuwa mamlaka husika zinapaswa kuwajibika na kuhakikisha ukweli wote kuhusu tukio hilo unajulikana.
Kauli ya Gachagua inajiri huku uchunguzi kuhusu kifo cha Victoria Mutiso ukiendelea.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































