#Football #Sports

KOCHA AKONNOR KUTATHMINI KIKOSI CHAKE CHA KWANZA BAADA YA CECAFA

Kocha wa Gor Mahia Charles Akonnor, amesema mashindano ya CECAFA Kagame Cup yamemsaidia kupata picha nzuri ya kikosi chake kipya anapojiandaa kwa msimu mpya wa ligi. Gor Mahia ilirejea Nairobi Jumamosi baada ya kumaliza kampeni yake ya kikanda.

Mabingwa hao wa Kenya walipoteza fainali kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya wenyeji Rayon Sports katika muda wa ziada Ijumaa, kwenye Uwanja wa Amahoro. Licha ya kukosa taji hilo, Akonnor amesema mashindano hayo yamekuwa muhimu kwake.

Kocha huyo amesema mechi tano walizocheza zimemsaidia kuwatathmini wachezaji wapya, kujaribu mipangilio tofauti ya kikosi na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho. Gor Mahia sasa inaendelea na maandalizi ya msimu mpya, huku ikilenga kuimarika zaidi.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *