WASHUKIWA WA MAUAJI YA VICTORIA MUTISO KUENDELEA KUZUILIWA
Washukiwa watatu wa mauajia ya Daktari wa Ubongo Victoria Mutiso wamefikishwa katika mahakama ya milimani jijini Nairobi huku maafisa wa idara ya upelelezi wa kesi za jinai DCI wakiomba mahakama iwaruhusu kuwazuilia kwa siku 30 zaidi washukiwa hao ili kukamilisha uchunguzi.
Watuhumiwa hao ni Constable Elijah Kibelion, mwendashaji boda boda Daniel Mwangi na Kevin Ngugi Kinuthia wanaodaiwa kuwa kiunganishi muhimu katika mauaji hayo.
DCI inataka washukiwa hao wazuiliwe katika vituo mbali mbali vya polisi jijini Nairobi wakati wa kipindi kizima cha uchunguzi huku wakisema maafisa wengine 2 wa polisi bado wanatafutwa kuhusiana na mauaji hayo.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































