WANAHARAKATI WAMTAKA IG KANJA KUJIUZULU
Baadhi ya wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu nchini wameandamana nje ya lengo la idara ya kitaifa ya polisi wakimtaka inspekta mkuu wa polisi Daglas Kanja kujiuzulu.
Wanaharakati hao wanansema hatua hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa visa vya ukatili wa polisi pamoja na vifo vya washukiwa wakiwa katika vituo vya polisi.
Pia wameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha maafisa wanaohusika na ukiukaji wa haki za kibinadamu wanawajibishwa kisheria.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































