NCIC YAMUITA KALUMA KUHUSU KAULI ZA KISIASA
Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano, NCIC, imemwita Mbunge wa Homa Bay Mjini, Peter Kaluma, kufika mbele yake kuhusu kauli za kisiasa anazodaiwa kutoa katika Kaunti ya Homa Bay kabla ya mkutano wa Linda Mwananchi.
Kaluma ametakiwa kufika katika afisi za NCIC hapo kesho mwendo wa saa nne asubuhi, ili kusaidia katika uchunguzi unaohusiana na kauli anazodaiwa kutoa Agosti 15 mwaka huu.
Mwito huo umetolewa chini ya Sheria ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano, huku Kaluma akitarajiwa kutoa maelezo yake kwa tume hiyo kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































