HOMEBOYZ YAONYESHA IMANI KWA KOCHA EDWARD MANOAH
Meneja wa Kakamega Homeboyz Boniface Imbenzi amemuunga mkono kocha mpya Edward Manoah kuiongoza timu hiyo kufanya vizuri katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Kenya.
Imbenzi amesema uteuzi wa Manoah unalenga kubadili matokeo yasiyoridhisha ya misimu iliyopita, huku kocha huyo akisaidiwa na Paul Okatwa mwenye uzoefu wa kufanya kazi katika klabu hiyo hapo awali.
Amesema Okatwa amewahi kufanya kazi pamoja na makocha Francis Baraza na Patrick Odhiambo, jambo analoamini litasaidia benchi jipya la ufundi kuimarisha kikosi na kurejesha Homeboyz katika ushindani wa juu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































