#Local News

SERIKALI KUAGIZA MAGUNIA MILIONI 25  YA MAHINDI NCHINI

Serikali imetangaza mpango wa kuagiza magunia milioni 25 ya mahindi, kila moja likiwa na uzito wa kilo 90, ili kukabiliana na upungufu wa chakula unaoweza kusababishwa na ukame na athari za mabadiliko ya tabianchi

Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amesema serikali tayari imeweka mipango ya kuwezesha uagizaji wa mahindi hayo, huku akiwahakikishia Wakenya kuwa hatua madhubuti zimechukuliwa kuhakikisha hakuna uhaba wa chakula nchini

Kagwe amesema uagizaji huo unalenga kuongeza akiba ya mahindi nchini na kuziba pengo linaloweza kujitokeza kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa chakula kufuatia ukame na changamoto za hali ya hewa.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *