#Local News

SAKAJA AELEZA MPANGO WA KUJIUNGA NA ODM

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amethibitisha kuwa anaendelea na mazungumzo kuhusu uwezekano wa kujiunga na chama cha ODM na kujiondoa katika chama tawala cha UDA.

Sakaja amesema kwa sasa anafanya mashauriano na wahusika mbalimbali kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho, akisisitiza kuwa anataka kufanya uamuzi ulio na msingi mzuri.

Gavana huyo amesema mpango huo umekuwa ukijadiliwa kwa muda kutokana na uhusiano wake na mwanzilishi wa ODM, marehemu Raila Odinga, akisema kwa muda mrefu amekuwa na shauku ya kujiunga na chama hicho.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *